Saturday, June 7, 2014

Muigizaji maarufu Tanzania Mzee Small, amefariki dunia. Chanzo cha taarifa hizi ni Mtoto wake wa kiume Mahmudu (Mongamba) ambae amenipigia simu sasa hivi muda ni saa 7 usiku.

Anasema Baba yake alipelekwa hospitali ya Muhimbili Jumamosi Tar 7 yani jana, muda wa saa mbili asubuhi baada ya kuzidiwa.

Ameeleza kwamba alishinda nae kutwa nzima ila ilivofika saa 4:09 usiku akafariki akiwa mikononi mwake.

Mzee small alikua anasumbuliwa na tatizo la kupooza kwa muda mrefu. Mara ya mwisho mimi binafsi kumuona, nilienda kwake na Bambo, Zembwela pamoja na Team ya HOTMIX ya East Africa Television kumfania mahojiano.

Alikua amechangamka lakini alikua anapoteza kumbukumbu kila anapoongea kwa muda mfupi.

Sina ripoti zaidi ya hiyo kuhusu kilichosababisha kifo chake.

Msiba wa Mzee small upo nyumbani kwake Tabata Mawenzi. Mungu ampumzishe kwa amani.
source.michaeli lukindo

No comments:

Post a Comment