kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii kinyume na taratibu onyo hili kutoka kwa jeshi la polisi linakufaa .pitia hapa.....,,,,,,,
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera
Senso akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Septemba
3,2014 kuhusu kupiga marufuku watu wanaotumia mitandao kinyume na
taratibu
JESHI la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya
ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na
kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri.
Akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3,2014 Msemaji wa Polisi, Advera
Senso alisema kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.
"Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na
simu za kiganjani kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza
taarifa za uchochezi,kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali.
"Wengine wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali
ambayo ni kosa la jina, ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya
hivyo ni kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.
Senso aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa
kutoifahamu si sehemu ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria,
atakabainika kutenda kosa hilo bila kujali anaifahamu sheria au la,
atachukuliwa adhabu kali.
Alisema oparesheni ya kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi
nzima kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa
lengo la kuwakamata waharifu wa aina hiyo.
Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia
mitandao kufanya utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini
sanjari na blogs zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.
"Wapo baadhi ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na
kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi
la polisi na yeyote atayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake,"
alisema.
Hivyo alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha
na uharifu huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza
kwa wengine bali waufute.
Pia aliziomba kampuni za simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina
hiyo wasiruhusu uende kwa mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na
uovu huo.
No comments:
Post a Comment