Tuesday, September 2, 2014

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI NYUMBA ZA MAKAZI ZA MEDELI

1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wenye nyumba 150, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)
2Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wengine wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC, Nehemia Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji.
3Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wenye nyumba 150, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye. 4Majengo ya Nyumba za Makazi za Medeli Mjini Dodoma kama yanavyoonekana pichani. 5Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji huku Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene wakishuhudia wakati wa ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma. Mradi una jumla ya nyumba 150. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa) 6Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Meneja wa NHC katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Bulla Boma wakati wa ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma. 7Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mara baada ya ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment