TAZAMA TUKIO ZIMA LA AJALI YA HELKOPITA ILIOMPATA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI JOSHUA NASSARI
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amenusurika kifo
baada ya ndege aina ya helikopita aliyokuwa amepanda kudondoka akiwa
katika ziara katika jimbo lake lilipo mkoani Arusha.
Hakuna aliyepoteza
maisha katika ajali hiyo, na Mbunge Nassari pamoja na Rubani wake wako
Hospitali ya Seriani mkoani Arusha kwa matibabu baada ya kupata majeraha kwenye ajali hiyo.
Joshua Nassari pamoja na
abiria wengine wawili na rubani wao wamenusurika kifo baada ya helkopta
waliyokuwa wakisafiria kuhamasisha uandikishaji Jimboni kuanguka jioni Taarifa zinaeleza kuwa helkopta hiyo imeanguka katika kijiji cha Leguruki Wilayani Arumeru Mashariki baada ya hali ya hewa kuwa mbaya.
Nassari na majeruhi wengine wamewahishwa hospitali ya Selian Jijini Arusha kwa matibabu ya majeraha kiasi waliyoyapata.
Blog hii inaendelea kufuatilia tukio hili kwa karibu na kukujuza kila kitu.
No comments:
Post a Comment