Akizungumza katika chuo hicho principal and CEO of Danish &;camp; Tanzania Training Centre For Development Cooperation MS TCDC in Arusha.Dr Suma Kaare katika kongamano la vijana wa Afrika Mashariki "YOUTH GOVERNANCE FESTIVAL" amesema kwamba vijana hao wataweza kujadiliana ikiwemo mtangamano wa Afrika Mashariki na kuweza kutoshiriki katika masuala mbalimbali ambayo yatawaharibia maisha
Amesema kwamba vijana hao wamedhamiria kutoa maazimio kama vile amani baina ya jumuiya ya madola na kutoa mikakati yao kama vijana katika masuala mbalimbali ambayo yatawapa miongozo ambayo itabeba dhamira ya dhati katika kujikomboa
kwenye picha ni principal and CEO of Danish &camp; Tanzania Training Centre For Development Cooperation MS TCDC in Arusha.Dr Suma Kaare
Akizungumza katika ufunguzi huo mkuu wa wilaya ya Arumeru mh Nyirembe Munasa alisema kwamba ni vyema vijana wakaonyeshwa fursa mbalimbali na kushirikishwa katika ngazi za uongozi ili kuweza kuwa na mawazo mapya ambayo yatachoche ufanisi wa kazi
mkuu wa wilaya ya Arumeru mh Nyirembe Munasa kushoto akifafanua jambo ,katikakati mbunge wa arumeru mashariki na kulia ni Dr suma Kaare
Ameongeza kwamba vijana wengi wamekuwa wakihitimu vyuo mbalimbali pasipo kujua ni fursa gani zinatakiwa kutumika ili kujikimu na badala yake wanatakiwa kujishughulisha na ujasiriamali ili kuweza kuwa na dira itakayoweza kuwakwamua kiuchumi
Nyirembe amesema kuwa vijana wanatakiwa kujitolea kufanya kazi katika ofisi za serikali ili kuweza kujijengea uwezo ambao utawasaidia kupata nafasi za kuajiriwa ili kuweza kuongeza utendaji kazi katika uongozi
Mratibu wa kongamano hilo Nassor Yusuph Mdemu amesema kwamba vijana wengi wanashindwa kutumia fursa wanazozipata kutokana nakutokuwa na uzoefu wa kufanya kazi katika nyanja za kisiasa,kiuchumi,kiutawala Pamoja na kiutamaduni hivyo kupitia jukwaa lao la Afrika mashariki litawapa nafasi yakuzungumza masuala yao nakupatiwa ufumbuzi
Ameongeza kwamba vijana wengi waliopo mitaani wanatakiwa kuelimishwa na kujitahidi kupatiwa elimu ambayo itawajenga nakuwasaidia kuendeleza maisha hayo
Mratibu wa kongamano hilo Nassor Yusuph Mdemu aliyevaa sweta jekundu akiwa na washiriki wenzake katika kongamano hilo linaloendelea chuoni hapo
Kongamano hilolimeanza jumatatu na litahitimishwa siku ya ijumaa ambapo vijana watajadili na kupambanua mambo mbalimbali na kuweza kuzipatioa ufumbuzi ambao utawajenga katika maisha yako ya kila siku
Story & picha zote na Godfrey Thomas
No comments:
Post a Comment