Sunday, November 2, 2014


Pichani ni Mzee Warioba akitolewa nje baada ya vurugu zilizojitokeza katika Mdahalo wa "Mchakato wa Katiba Mpya, Maoni ya Wananchi na Katiba Inayopendekezwa" yaliyofanyika mapema leo hii Ubungo Plaza.

VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea jioni ya leo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.

Inaelezwa kuwa vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.

No comments:

Post a Comment