Saturday, May 23, 2015

Chama cha waalimu C.W.T kinataraji kufanya uchaguzi wake mkuu tarehe 28 mwezi huu


Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT)  Ezekiah Oluoch akizungumza juu ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kitaifa utakaofanyika Mei 28 katika mkutano Mkuu wa chama hicho utakaofanyika Mei 25 mpaka 28 katika ukumbi wa mikutano wa Ngurudoto,katika mkutano wake na waandishi wa habari jana uliofanyika katika ofisi za mkoa za chama hicho,kushoto ni Katibu wa chama mkoa Hassan Said,










 Na,Godfrey Thomas_Arusha


Chama cha waalimu cwt taifa kinataraji kufanya uchaguziwake tarehe 28 mwezi huu katika ukumbi wa mikutano wa ngurudoto uliopo jijini arusha nakuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka hapa nchini Tanzania

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT)  Ezekiah Oluoch amesema kwamba wagombea katika nafasi mbalimbali wameongezea kuanzia ngazi ya Raisi wa chama hicho Ambavyo hivi sasa anayeshikilia nafasi hiyo ni Mwalimu Gratian Mukoba

Oluouch amesema kwamba maandalizi ya uchaguzi mkuu yamekwisha kukamilika hivyo waalimu wanatakiwa kujiamini na watakapofika jijini Arusha wanatakiwa kuwa na vitambulisho vyao vya kazi pamoja na bima za afya kwa ajili ya kujirahisishia ulinzi zaidi

Kwa upande wa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa arusha Mwalimu juvin Duruya Kuyenga Amesema kwamba mgeni rasmi Anatarajiwa kuwa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh Jakaya Mrisho Kikwete

Ameongeza kwamba chama hicho kimejipanga vizur ambapo kitatoa demokrasia ya wagomgea kumchagua kiongozi wanayemuhitaji na kwamba katika ngazi zote za chini kiuongozi zimeshapata viongozi hivyo kilichobaki ni uchaguzi mkuu pekeee pamoja na kujadili ajenda mbalimbali za chama hicho

Aidha mkutano unataraji kuanza tarehe 26.5.2015 nakuhitimishwa tarehe 28 kwa uchaguzi mkuu

No comments:

Post a Comment