Friday, July 24, 2015

MBUNGE WA KARATU MCH.ISRAEL NATSE AWAAGA WANANCHI QAMBALA KUPEPERUSHA BENDERA

Mbunge mstaafu wa Jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Mchungaji Israel Natse akizungumza katika mkutano mkuu wa Jimbo hilo ambao ulifanya uchaguzi wa madiwani na Wabunge wa  Viti Maalumu mgombe Ubunge wa Jimbo la Karatu,katikati ni Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalisti Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Karatu,Thomas Darabe.

Mbunge wa Viti Maalumu wilaya ya Karatu,Cecilia Paresso akizungumza katika mkutano huo ambao alichaguliwa na wajumbe wanawake kuwania nafasi hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.

Mwanamke wa kwanza kuwahi kujitokeza kuomba ridhaa ya wanachama kumchagua kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Karatu,Fransisca Duwe akijinadi kwa wajumbe.

Willy Qamballa mmoja wa wagombea akijinadi kwa wajumbe

Aliyekua Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karatu,Lazaro Maasay akiomba kura kwa wajumbe

Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akiwashukuru wajumbe baada ya kujizolea kura 217 na mpinzani wake wa karibu Lazaro alipata kura 84.

Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akifurahia na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi.

No comments:

Post a Comment