TASWIRA: MKUTANO WA CHADEMA MWANZA
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa
akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza waliohudhuria katika mkutano mkubwa
uliofanyika jijini hapo jana.
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa CHADEMA Mh Tundu LISSU akiwahutubia wakazi wa Mwanza jana.
Mbunge wa Viti Maalum Kutoka mkoa wa
MARA aliyehamia CHADEMA kutoka CCM Mh Esther Bulaya akihutubia katika
mkutano mkubwa jijini Mwanza jana.
Mbunge wa Nyamagana Mh Ezekiah Wenje akihutubia katika mkutano jijini Mwanza.
Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA bara Mh
John Mnyika akiwa na Mbunge wa Kahama aliyejiunga na CHADEMA kutoka CCM
Mh James Lembeli wakiwapungia mikono wakazi wa Mwanza.
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Bara Prof
Abdallh Safari (aliyevaa miwani) akiongozana na Katibu Mkuu wa Chadema
Dr Wilbroad Slaa (katikati) na Mbunge wa Musoma mjini Mh Vicent
Nyerere(kushoto)
Waliokuwa wabunge wa CCM waliohamia CHADEMA mh James Lembeli (Kulia) na Mh Esther Bulaya (kushoto)
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Taifa
CHADEMA Mh Halima Mdee akiwa na Mh Esther Bulaya wakiwapungia mamia ya
wakazi wa Mwanza waliofika kuwalaki.
No comments:
Post a Comment