Friday, August 7, 2015

TFDA IMEJIPANGA KATIKA KUHAKIKISHA INAWATIA MBARONI WATAKAOHUSIKA NA KUUZA BIDHAA AMBAZO HAZIJAIDHINISHWA NA MAMLAKA HIYO


Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Hiit Sillo.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Hiit Sillo.

Na,Godfrey Thomas,Arusha
 
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imesema imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha inalinda afya ya mlaji kwa kuanzisha operesheni itakayowezesha kuwakamata watakaokiuka kanuni na taratibu za mamlaka hiyo

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Hiiti Siilo ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa sikukuu ya wakulima nane nane inayofanyika Mkoani Arusha

Sillo amesema kwamba kwa mwaka huu wameweza kufuta usajili wa aina tano za dawa za binadamu na kuamuru ziondolewe katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini kote mara moja kutokana na kubainika kuwa na viambata vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na wakati mwingine kusababisha vifo.

mkurugenzi mkuu mamlaka ya chakula na dawa TFDA Hiit Sillo amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya uchuguzi wa kitaalam uliofanywa kwa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO.

Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanatembelea banda lao linalopatikana katika viwanja vya taso ili kuweza kujionea bidhaa mbalimbali pamoja na kupata elimu zaidi juu ya mamlaka hiyo

Ameeleza kwamba TFDA imekuwa ikishirikiana na wananchi katika kuhakikisha inawafichua wale ambao wamekuwa wakihusika na mandao huo ambao unahatarisha afya za walaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini

No comments:

Post a Comment