Friday, October 30, 2015

MAGUFULI RAISI MTEULE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.John Pombe Magufuli hatimaye ndiye amefanikiwa kuwa rais mteule wa nchi ya Tanzania mara baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais uliofanyika october 25.
John Magufuli.jpg
 Dkt.John Pombe Magufuli 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva alitoa matokeo hayo mara baada ya kumaliza kutoa matokeo ya Uraisi kwa kila jimbo ambapo amesema kuwa Magufuli,alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema akijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote.


Aidha mara baada ya siku ya jana Dkt.Magufuli kutangazwa kuwa mshindi  wa Uraisi wa Tanzania siku ya leo 30/10/2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imempatia cheti cha ushindi huo


Magufuli
Magufuli akionyesha Cheti alichokabidhia mara baada ya kuibuka mshindi(picha na BBC)
Dkt  Magufuli amekabidhiwa cheti hicho kwenye hafla iliyoandaliwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Vile vile hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete ambaye anaondoka madarakani lakini pia walikuwapo waangalizi wa uchaguzi kutoka makundi mbalimbali hapa Duniani.

Huyu ni Mhe. Samiah Suluhu Hassan ambaye ndiye makamu wa Raisi mteule wa Tanzania Dkt Magufuli


Hata hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia aliyekuwa mgombea wao wa Urais Mhe Edward Ngoyai Lowassa kimepinga matokeo hayo ya kuchaguliwa Magufuli wakidai wamedhulumiwa  hali iliyopelekea hata kutofika wakati akipewa Cheti.


Kwenye uchaguzi huo, kati ya wapiga kura 23.24 waliojiandikisha, ni milioni 15.58   waliopiga kura, ambao ni sawa na asilimia 67.31 ya wapiga kura wote. 

No comments:

Post a Comment