Friday, October 30, 2015

TAKRIBAN WATU 27 JIJINI ARUSHA WAUGUA KIPINDUPINDU
ARUSHA 
Wito umetolewa kwa jamii pamoja na wafanyabiashara wa vyakula,maji na matunda jijini Arusah kuimarisha usafi katika maeneo yao ili kuepukana na ugonjwa hatari wa kipindupindu.

Cholera bacteria SEM.jpg
 Virusi vya Vibrio cholerae vinavyosababisha ugonjwa wa kipindupindu
 Akizungumza na Wanahabari ofisini kwake mkuu wa Wilaya ya Arusha ndg.Fadhili Nkurlu amesema kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kuibuka katika baadhi ya maeneo jijini hapa imepelekea kusababisha watu 27 kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Nkurlu amesema mpaka sasa wagonjwa watano wa ugonjwa wa kipindupindu wamelazwa katika hospitali ya levolosi huku wagonjwa hao wakitoka kwenye maeneo tofauti ambapo wagonjwa watatu wametoka mkoa wa Singida,mmoja kutoka halmashauri ya Arusha DC na halmashauri ya Simanjiro na wengine 22 wakitoka halmashauri ya jiji la Arusha.

"Maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo jijini hapa ni pamoja na kata yaKimandolu,Sinoni,Daraja mbili pamoja na Sombetini"amesema Nkurlu 

Ameeleza dalili mbalimbali za ugonjwa wa kipindupindu kuwa ni pamoja na kuharisha kwa ghafla,kutapika lakini pia mgonjwa kuishiwa na maji mwilini hali inayosababisha mgonjwa kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Arusha ndg.Juma Iddi amewataka wananchi kuhakikisha wanafata taratibu zilizosahihi katika kuboresha usafi kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kila wanapotoka chooni,kuepuka kula matunda ambayo hayajaoshwa na kunywa maji yasiyochemshwa.

Hata hivyo hivi karibuni maeneo mbalimbali hapa nchini yamekumbwa na mlipuko wa ugonjwa hatari wa kipindupindu ikiwemo mikoa ya Dar-es-salam,Morogoro,Pwani,na Kilimanjaro hivyo wananchi wametakiwa kuboresha usafi kwenye maeneo yao

No comments:

Post a Comment