Tuesday, May 24, 2016

Utatuzi wa mgogoro wa burundi umefikia katika hatua hizi





Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi raisi mstaafu wa Tanzania Benjamini wiliam mkapa amesema mgogoro wa kisiasa nchini Burundi umefikia katika hatua ya usuluhishi kutokana na pande zote kukubali kuacha mauaji ya raia nakukubali kuendelea kuirejesha Burundi katika hali ya ulinzi na usalama


Mkapa amesema kwamba kuna makundi ambayo bado wanaendelea kuwasiliana nayo ili kuhakikisha wanakuwa pamoja na kufikia makubaliano


 Raisi mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa alifungua mazungumzo ya kutafuta Suluhu katika mgogoro wa Burundi   ambao umedumu kwa muda mrefu May 21 na yamehitimishwa leo jijini Arusha

Mgogoro wa  kisiasa wa Burundi  umekuja  baada ya mgombea uraisi wa  awamu ya tatu Piere  Nkurunziza kugombea tena kwa kuvunja Katiba kinyume na utaratibu

No comments:

Post a Comment