MAJANGA ya moto kwa shule za sekondary Mkoani Arusha yamechukua sura mpya mara baada ya jeshi la polisi mkoani hapa kuibuka na kudai linawashikilia washukiwa wapatao 27 wakiwemo Wanafunzi, Walimu pamoja na Rai wa kawaida wakihushishwa na matukio ya kuchoma moto shule 6 huku likiendelea kusaka mfadhili wa mtandao huo wa kialifu.
Aidha katika tukio jingine lilotokea majira ya saa nane za usiku kuamkia jana shule Binafsi ya Sekondary ya Winning Spirit iliyopo katika kata ya Kiranyi imeteketea kwa moto ikiwa ni muendelezo wa matukio mbali mbali ya uchomaji wa shule yanayofanywa na watu wasiofahamika.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani hapa Charles Mkumbo alisema kuwa matukio hayo yalianza kujitokeza kuanzia Julai 31 mwaka huu ambapo shule mbali mbali toka wilaya za Munduli, Karatu, Longido, Arumeru na Arusha Dc zimeathiriwa na matukio hayo.
No comments:
Post a Comment