Monday, September 5, 2016

Sudani kusini rasmi jumuiya ya Afrika Mashariki



Nchi ya Sudani Kusini  leo September 5 imesaini hati ya makubaliano ambayo imeiruhusu nchi hiyo rasmi kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki Tayari kwa kuanza utekelezaji wa majukumu ya jumuiya hiyo

September 5 mwaka huu Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Agustine  Mahiga amesema hatua walizofikia ni za mwisho baada ya baraza la mawaziri kukubaliana mwezi Aprili mwaka huu na baadae kusaini mkataba wakujiunga

 Hati hiyo ya makubaliano imesainiwa na katibu mkuu wa jumuiya hiyo Liberat Mfumukeko na mshauri wa raisi wa sudani kwenye masuala ya uchumi Aggrey Tisa Sabuni

No comments:

Post a Comment