Monday, October 31, 2016

Maagizo ya mkuu wa wilaya ya Arusha kuhusu huduma kwa wazee

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel F. Daqarro ameagiza  Kabla ya mwaka kuisha idara ya afya  ya jiji ishughulikie ili wazee waweze   kupata  vitambulisho vya afya ilikuweza kuhudumiwa kiurahisi

Mkuu wa wilaya akiongozana na katibu tawala wa wilaya David Mwakiposa wameweza kukutana na wazee wa wilaya ya Arusha  katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano (AICC) nakusikiliza kero zao huku wakiahidi yale waliyokubaliana watayafanyia kazi

Kwa upande wa samweli ambaye ni mzee aliyeshiriki katika mkutano huo ameseimu jitihada zilizofanywa na mkuu wa wilaya nakusema haijawahi kutokea kwa viongozi kukutana na wazee kwa ajili yakusikiliza kero zao

Aidha amewataka viongozi hao kusimamia falsafa ya mwalimu nyerere yakufanya kazi,kwa kufuata maadili ili kuweza kusaidia taifa kusonga mbele



No comments:

Post a Comment