Thursday, October 6, 2016
Maamuzi ya mkuu wa wilaya ya Arusha leo baada yakufanya ziara katika soko la Samunge
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqqaro amefanya ziara katika soko la Samunge NMC Arusha kusikiliza kero za wafanyabiashara wa soko hilo nakukumbana na changamoto kadhaa ikiwemo suala la ulinzi wa soko hilo,umeme pamoja na suala la maji ambapo baada yakusikiliza kero hizo ameagiza Afisa biashara wa jiji pamoja na meneja wa soko hilo kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto hizo mara moja
Gabriel akiwa ameambatana na katibu tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amewataka watendaji wa eneo hilo kuhakikisha wanatatua migogoro iliyopo nabadala yake kutosubiri hadi viongozi wa juu kuja kutolea maamuzi masuala ambayo yapo ndani ya uwezo wao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment