Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqqaro leo september 30 amekutana na wadau pamoja na wafanyabiashara wa Arusha ambapo amesema kwamba atahakikisha anashirikiana nao katika kutekeleza majukumu mbalimbali hasa yakibiashara
Gabriel amesema kwamba ndani ya wiki moja atakutana na watumishi wanaohusika na wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga ili kuweza kuandaa utaratibu wakisayansi utakaowezesha kupangiwa eneo maalumu kwa ajili yakufanyia biashara
Ameongeza kwamba kutokana na kuwepo kwa suala la ufungaji wa maduka no vyema kila upande ukajitathimini ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kulipa kodi nakuwa na mashine za EFDs zitakazowezesha serikali kupata mapato yatakayosaidia wananchi kupata maendeleo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment