Idadi ya waalimu waliokuwa wakidai fedha kwa jiji la Arusha imefikia 701 ambapo leo september 23 imeeleza kulipwa wote milioni 169
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro akizungumza na vyombo vya habari amesema fedha zote zimekwisha lipwa kwa wakati na hakuna mwalimu yeyote anayedai katika jiji la Arusha
Gabriel amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga katika kuhakikisha inasimamia masuala yote ya msingi ikiwemo waalimu ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta stahiki zao nakutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo lililotaka waalimu kulipwa
Ameongeza kwamba baada ya mkuu wa mkoa kuwabana madiwani ambao walikuwa wakijilipa fedha kinyume na utaratibu zimepatikana nakupelekea waalimu kulipwa
No comments:
Post a Comment