Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekutana na waandishi wa habari leo September 21 nakuwaeleza kuhusiana na mkutano wa wadau wa utalii utakaofanyika kesho huku mgeni rasmi akiwa waziri wa maliasili na utalii Prof Jumanne Maghembe utakaofanyika kesho september 22 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa AICC
Gambo amesema utalii kwa mkoa wa Arusha umekuwa kwa kiwango kikubwa kutokana na wageni kutoka sehemu mbalimbali kuja kutazama vivutio vilivyopo kwa kuwa ni sehemu pekee ambapo vinapatikana,ameongeza mkutano huo utajadili hali ya maendeleo ya utalii ya mkoa,fursa zilizopo,mafanikio na changamoto nakuweka mikakati mbalimbali yakuboresha sekta ya utalii,Amewaomba wananchi na wadau kufika ili kujadili kwa pamoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment