Thursday, February 16, 2017

SIMBA YATINGA ROBO FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

Image result for Laudit Mavugo
 Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC ya Dar es salaam imeinyamazisha timu ya African Lyon kwa kuibanjua bao moja kwa sufuri(1-0) katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliochezwa  kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Kombe hilo ambalo ni maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) timu zote zilikuwa zinashambuliana kwa ushindani mkubwa lakini bahati ikaiendea timu ya Simba kwa kujipatia bao hilo la pekee lililopachikwa kimiani na mchezaji wa Kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo katika dkk ya 57.
Kwa matokeo hayo yameifanya timu ya Simba kutinga hatua ya Robo fainali ya kombe hilo.

No comments:

Post a Comment