Saturday, March 4, 2017

Lema kaachiwa kwa dhamana

Image may contain: 5 people, people sitting and outdoorHatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema baada ya kusota gerezani Tangu November Mwaka jana
.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja za pande zote mbili zilizowasilishwa mahakamani hapo leo na kuamua kuzitupitilia mbali hoja za upande wa serikali za kumnyima Lema dhamana.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache kupita tangu mahakama rufaa kutupilia mbali rufaa ya jamhuri, huku ikishangazwa na hatua ya Lema kukosa dhama hadi wakati huo.
Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1

"Ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa chama na wananchi wote waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke wangu, kama ningepata nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto wangu alifikia hatua akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na mimi gerezani, na akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani" Amesema Lema

Mwenyekiti wa  CHADEMA  Freeman Mbowe, amelaani nguvu iliyotumiwa na jeshi la polisi siku ya leo ya kuwapiga, kuwakamata na kuwatawanya wafuasi wa chama hicho waliofika mahakamani hapo kufuatilia kesi ya mbunge wao, huku akitangaza kuwa kwa leo hakutakuwa na tukio lolote la kisiasa mpaka watakapotangaziwa tena. 

No comments:

Post a Comment