Katika
hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa
nadra bungeni, Edward Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha
kuweka vipaumbele vingi visivyotekelezeka kwa wakati.
Alitaka serikali kuweka nguvu katika vipengele vichache vya msingi kama ajira, afya, elimu na miundombinu.
Aliwapongeza
mawaziri John Magufuli kwa kuimarisha barabara na Dk. Harrison
Mwakyembe kwa kubuni mbinu za kupunguza foleni jijini Dar es Salaam,
alizosema zinachangia kuharibu uchumi kwani watu wengi wanakaa
barabarani badala ya kufanya kazi.

No comments:
Post a Comment