Kikao kinachojadili maendeleo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Kanda ya ziwa Mashariki (Mara,Simiyu na Shinyanga) kimemtimua Mbunge wa
Maswa Magharibi John Magale Shibuda baada ya kupiga kura ya kutokuwa
na imani naye muda mfupi uliopita jioni hii.
Shibuda ambaye alihudhuria kikao hichou kama mbunge wa Kanda hiyo
alijikuta akipatwa na zahama hiyo baada ya mjumbe mmoja kutoa hoja kwa
Mwenyekiti wa Kikao hicho
Mjumbe huyo alisema Shibuda ni mamluki na kibaraka wa CCM hasa kutokana
na matamshi yake kadhaa dhidi ya Chadema na mwenendo wake usioridhisha
ndani ya chama.Aliongeza kwamba Shibuda alikuwa kwenye kikao hicho kwa
lengo maalum la kukusanya habari na kupeleka CCM.
Hatimaye hoja ya mjumbe huyo iliungwa mkono na wajumbe wote na hatimaye ikapigwa kura ya kutokuwa na imani naye.
Shibuda alikubali kuondoka ndani ya kikao hicho kwa aibu kubwa na hatimaye mkutano umeendelea.
CHANZO http://www.jamiiforums.com
No comments:
Post a Comment