Monday, December 2, 2013

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wilium Mkapa ameitaka jamii
kuacha kuendekeza zaidi maswala ya kisiasa ambayo yanaweka tofauti  na
badala yake wajikite  katika maswala ya kumwabudu mwenyenzi mungu na
kushiriki katika ujenzi wa nyumba za mungu ili kendeleza amani na
utulivu hapa nchini.

Mkapa aliyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika harambee
ya kuchangia ujenzi wa kanisa(sadaka maalum)katika kanisa  la parokia
ya Mtakatifu Vicent Pallot lililopo maeneo ya esso mjini hapa,ambapo
kiasi cha shilingi milioni 160 huku akichangia shilingi milioni 10.

Alisema kuwa ni vema jamii ikajenga taratibu za kupendana na kuachana
na maswala ya kuendekeza zaidi  siasa kwa kuwa yanawafanya kuwa na
tofauti ambazo hazimpendezi mungu mbele zake.

“sisi sote ni ndugu na ni waja wa mungu hatupaswi kugawana kwa ajili
ya tofauti zetu ila tunapaswa tushikamane ,tuwe wamoja na tusameheane
ndipo tutaweza kuleta amani katika nchi yetu”alisema Mkapa.

Aliongeza kuwa upendo,toba na msamaha katika nchi ya Tanzania ndio
silaha muhimu sana katika maisha ya watu hivyo ni vema wakahakikisha
kuwa wanaachana na sifa ambazo hazijengi jamii na zenye lengo la
kupotosha.

Aidha alilitaka kanisa la katoliki Tanzania kuhakikisha kuwa linakuwa
na utaratibu wa kuendeleza ujenzi wa makanisa hapa nchini kwani hapo
kabla kanisa hilo halikuwa na mwamko huo wa kujenga makanisa na badala
yake lilitegemea wafadhili wan je na yale yaliyoachwa na wamisionali
zaidi.

Kwaupande wake Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Arusha,
Josephat Lebulu aliwataka wakristo kuwa na  mshikamano,kwani kanisa
haliwezi kukua na kusonga mbele katika kazi ya  bwana  hivyo ni vema
wakahakikisha kuwa wanaweka tofauti zao pembeni na kushikana kwa
pamoja.

Aidha alisistiza kuwa wao kama kanisa wataendelea kuliombea kanisa ili
amani na mshikamano uendelee kuwepo ambapo aliwaasa viongozi kuondoa
utofauti wao walionao na badala yake wawe kitu kimoja kwa kuyatenda
yale yapasayo haki .

Naye Paroko wa kanisa hilo,Father Andrea Kahumbia alisema parokia hiyo
ina umri wa miaka saba tangu kuanzishwa na kwamba ujenzi wa kanisa
hilo jipya unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.2 na hatua ya awali
imeshakamilika na hivyo kiasi cha shilingi milioni 500 zinahitajika
ili kukamilisha ujenzi huo ambapo likikamilika litakuwa na uwezo wa
kuingiza waumini 1600 kwa awamu moja.

Aliwataka mapadri wenzake kusimamia majukumu na nafasi zao kikamilifu
hususan kazi yao ya uinjilishaji na kuzidi kuonyesha ushirikiano kwa
waumini ili kazi ya mungu izidi kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment