Watu watatu
wanaodhaniwa kuwa majambazi wameuwawa kwa kupigwa risasi na askari polisi
katika eneo la Engosheraton mkoani Arusha.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, naibu Kamishna
mwandamizi wa polisi Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema watuhumiwa hao wameuwawa wakati wa
majibishano ya risasi na askari polisi waliokuwa nyumbani kwa wahalifu hao.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, naibu Kamishna
mwandamizi wa polisi Liberatus Sabas akiwa amesheka moja kati ya zana ya kihalifu waliowashika nayo hao wahalifu
Amesema
mnamo tar.27/2/2016 majira ya asubuhi jeshi la polisi jijini hapa
walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa eneo hilo la Engosheraton
Sinon kuna kijana mmoja wanamtilia shaka kuwa anajihusisha na matukio ya
uhalifu.
Amesema
jeshi la polisi liliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Athumani
Ramadhani na alipopekuliwa alikutwa na milipuko ya aina ya TMV6
WATER
EXPLOSIVE 17 GIOGEL KUBELA 10,makoti makubwa 2 pamoja na kofia moja ya
kuficha uso(mask) na baada ya kumfanyia mahojiano aliwaambia wenzake
wawili wanaoshirikiana.
Kamanda
Sabas amesema walipofika eneo walilopo wenzake alipiga kelele na
wakaanza kushambuliana na jeshi la polisi hivyo mpaka kufikia hatma ya
kuwashinda kwa kuwapiga risasi.
"Upekuzi
ulipofanyika katika chumba chao hao wahalifu wawili walikuta vitu
vifuatavyo Sare 5 za JWTZ(COMBAT),bunduki aina ya AK 47 ikiwa na risasi
18, pikipiki moja iliyobomolewa yenye namba bandia MC 983 BMK,Bendera 2
nyeusi zenye maandishi ya kiarabu zinazotumiwa na makundi ya kigaidi
pamoja na Kisanduku cha chuma"amesema kamanda Sabas.
vitu vya kihalifu vilivyokamatwa toka kwa wahalifu gao
Hata hivyo kamanda Sabas
amesema miili ya marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Maunt Meru kwa
ajili ya utambuzi wa ndugu na jamaa zao wa karibu.
No comments:
Post a Comment