Friday, April 26, 2013

ANGALIA PICHA ZA YULE MENEJA MZINZI ALIYEFUMANIWA NA MKE WA MTU AMEACHISHWA KAZI..







Katika habari hiyo, mtu aliyetajwa kwa jina la Everson Makowa (49) ambaye ni meneja wa kampuni ya kusafirisha mizigo ya Malawi Cargo tawi la mkoani hapa alidaiwa kunaswa gesti na mke wa mfanyakazi wake . 



Sasa, habari mpya ni kwamba bosi huyo ambaye pia ni mbunge mstaafu wa Jimbo la Nkotakota South East nchini mwake anadaiwa kupigwa chini kazini kwake baada ya uongozi wa kampuni hiyo makao makuu yaliyopo nchini Malawi kuzinyaka taarifa za kudaiwa kufumaniwa na mwanamke huyo.
 Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada ya habari hiyo kutoka mtandaoni, uongozi wa kampuni hiyo ulimwandikia barua ya kumwachisha kazi mtuhumiwa huyo.




Mwandishi  wetu Jumatano iliyopita alikwenda nyumbani kwa mdaiwa huyo ambapo pia ndiko zilipo ofisi za kampuni hiyo kwa lengo la kuzungumza naye lakini watu waliokuwepo walisema alikuwa ametoka.
 Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja alikiri jamaa huyo kutemeshwa mzigo na kuongeza kuwa, tayari bosi mwingine amefika kuziba nafasi yake. 
Mwandishi  wetu alipoomba azungumze na bosi mpya, aliambiwa alikuwa na wageni hivyo ikawa vigumu kumpata.
 Pamoja na habari ya kutemeshwa kazi, mtuhumiwa huyo ameshindwa kuondoka Mbeya kurudi Malawi kufuatia kesi inayomkabili kutarajiwa kuunguruma mahakamani ambapo mume wa mwanamke huyo ndiye mlalamikaji.




Siku ya tukio, majira ya saa 11:25 jioni, mtuhumiwa huyo alifika kwenye gesti hiyo akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 821 ASY.



CHANZO AUDIFACEBLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment