Mwanamuziki
gwiji nchini Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa
toka kwa familia yake zinasema Bi
Kidude aliekuwa akipatiwa matibabu
katika hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa
kama
mwanamuziki mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na
umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na
mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini
imepoteza moja ya nguzo kubwa.
Pumzika kwa amani
No comments:
Post a Comment