Hatua za haraka zimetakiwa
kuchukuliwa kuinusuru shule ya msingi OLCHOK iliyopo kijiji cha Siwandeti kata
ya Kiranyi halmashauri ya Arusha kukumbwa na magonjwa ya milipuko kutokana na
choo kilichokuwa kikitumiwa na wanafunzi
wa shule hiyo kodidimia na kupelekwa wanafunzi wa shule hiyo kujisaidia
vichakani.
Wakizungumza na mwandishi wa
habari hizi katika shule hiyo kujionea
hali halisi baadhi ya walimu na wakazi wanaoishi karibu na shule hiyo wamesema
kuwa choo hicho kilibomoka mnamo siku ya jumamosi usiku ambapo hadi leo hakuna hatua
yoyote iliyochukuliwa na kutafuta hata choo za dharura hivyo kupelekea
wanafunzi zaidi ya 2000 na walimu kugombania choo kimoja chenye matundu matatu
huku wengine wakijisaidia vichakani na kupelekea hali ya ufundishaji katika
shule hiyo kuzorota
Naye mwalimu mwingine
ambae Akutaka jina lake litajwe redioni amesema kuwa kilichopelekea choo hicho
kubomoka ni kujengwa chini ya kiwango
Kufuatia hali hiyo afisa
elimu wa halmashauri ya Arusha vijijini ameombwa kufunga shule hiyo ya Olchok kwa muda hadi pale ufumbuzi wa kupatikana kwa
choo kingine ili kuzuia magonjwa ya milipuko kuikumba shule hiyo
Kwa upande wake mkuu wa
shule hiyo bwana boniphance dikumwe amesema kua wapo katika mikakati ya
kukutana na wanakiji pamoja na viongozi kuangalia atma ya shule hiyo kupata
choo kwani wanafunzi wapo katika wakati mgumu kiafya
Ataivyo wananchi walisema
kua almashauri ilitenga pesa kiasi cha shilingi million mia nne kujenga vyoo
vya kisasa lakini pesa hizo azikufanya kazi iyo na badalayake pesa izo
zilitumika kununulia bomba moja la nchi mbili nakuambiwa zimekwisha na kutupia
lawama kamati ya shule na afisa mtendaji wa kijiji kutochukua atua yoyote hile
No comments:
Post a Comment