Friday, April 19, 2013

WANAOTUMIA LAINI ZA SIMU ZISIZOSAJILIWA KUTOZWA 500, AU KUFUNGWA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ), Profesa  John Nkoma, akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na viongozi wa Kampuni za Simu kuhusu usajili wa laini za simu Dar es Salaam 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.
‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano   mteja au muuzaji wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Katika maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza au kutoa namba za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na adhabu yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha miezi 12.

Profesa Nkoma alisema kwa kushirikiana na kampuni za simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu ili kuwabaini wanaohusika na uvunjifu wa sheria kwa lengo kuwalinda watumiaji wema, jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na usawa katika  jamii.
Pia alisema mikakati iliyopo ya TCRA simu ambazo hazijasajiliwa hazitafanya kazi, hivyo watu  ambao hawajajisajili waanze mchakato huo.
CHANZO MWANANCHI

No comments:

Post a Comment