Mrembo huyu aliyejitambulisha
kwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimojawapo mjini Iringa akilia baada
ya kupokea kichapo kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara eneo la
Miyomboni mjini Iringa baada ya kuiba viatu vya mtumba na kuficha
kwapani.....
Hapa akimpigia simu mpenzi wake ili aweze kumkomboa baada ya kutakiwa kulipa Tsh 50,000 kwa viatu pea mbili alizoiba .
----------------------------------------------------
Tukio la
mrembo huyo kupokea kichapo na kuvuliwa nguo na kupokonywa simu
yake na mikoba zaidi ya mitano pamoja na kiasi cha TSh 15,000 ambazo
alikuwa amezihifadhi limetokea jumapili wiki hii katika eneo la
Miyomboni mjini Iringa.
Akielezea juu ya mkasa huo wa aina
yake leo mfanyabiashara huyo mama Masawe alisema kuwa eneo hilo
amekuwa na kawaida ya kuibiwa viatu katika duka lake la viatu vya
mtumba .....
Mama huyu anadai kuwa mbali ya
kukamatwa kwa mrembo huyo bado amepata kukamata vijana zaidi ya
wawili watanashati ambao wamekuwa wakifika na kujifanya wakichagua
viatu na kuishia kuiba na kutoweka .
Binti huyo ambaye ni mwanachuo alifika dukani hapo na kuanza kuchagua viatu akijifanya ni mteja .....
Baada ya kuona muuza duka
ameangalia pembeni, binti huyo alichukua pea mbili za viatu
na kuzificha kwapani asijue kwamba pembeni kulikuwa na mtu
mwingine aliyekuwa akimwangalia....
Alipoaga na kutaka kuondoka ndipo
timbwili la kichapo lilipoanza kwa mrembo huyo ambae aliomba
asipelekwe polisi na asipewe adhabu kubwa kwa kuwa ana
ujauzito wa miezi mitatu tumboni.
Alisema kuwa kutokana na maombi ya
mrembo huyo kupunguziwa adhabu hakuweza kumfikisha polisi zaidi ya
kumpa kichapo cha kufa mtu na kumpokonya mali zote alizokuwa ametoka
kuiba katika maduka ya Miyomboni mjini hapa pamoja na simu yake ya
kiganjani .
CHANZO SHADDYBLOG
No comments:
Post a Comment