Monday, April 22, 2013
China yatoa taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Marekani
Ofisi ya habari ya serikali ya China imetoa taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Marekani mwaka 2012, ikiwa ni majibu ya taarifa kama hiyo iliyotolewa hivi karibuni na Marekani ambayo imepotosha ukweli na kuishutumu China kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo
.
Taarifa iliyotolewa na China inasema, kwenye taarifa yake, Marekani inazituhumu nchi zaidi ya 190 kwa kukiuka haki za binadamu, huku ikikaa kimya kuhusu hali mbaya yaukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo..
Taarifa hiyo imetaja maeneo sita ambayo haki za biandamu zinakiukwa nchini Marekani, kama vile usalama, haki za uraia na haki za kushiriki kwenye mambo ya siasa, haki za kushiriki mambo ya uchumi na ya jamii, ubaguzi wa rangi, haki za wanawake na watoto, pamoja na matukio ya kuingilia haki za bindamau katika nchi nyingine.
Hii ni mara ya 14 kwa China kutangaza taarifa kama hiyo, ikijibu taarifa inayotolewa kila mwaka na Marekani kuhusu hali ya haki za binadamu katika nchi mbalimbali duniani
CHANZO CHINA SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment