Rais mstaafu wa Afrika Kusini
Nelson Mandela anaendelea kupata nafuu wakati akitibiwa homa ya mapafu,
kwa mujibu wa madaktari wake.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, ilisema kuwa Mandela alitembelewa na jamaa zake wakati akiendelea kupokea matibabu.Inaarifiwa kwa sasa hali yake inaendelea kuwa nzuri ikilinganishwa na alivyokuwa wakati alipolazwa hospitalini tarehe 27 mwezi Machi
Mandela amelazwa hospitalini sasa kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Mnamo Disemba alitibiwa homa ya mapafu na kibofu na alikaa hospitalini sana kuliko wakatii mwingine wowote.
Mnamo Februari alitibiwa maradhi ya tumbo.
Wiki jana rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 94,pia alibitiwa maradhi ya mapafu.
Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu muda atakaosalia kuwa hospitalini.
Bwana Mandela alikuwa rais wa Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi 1999 na anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa hilo kwa kupigana dhidi ya enzi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Licha ya kufungwa kwa miaka mingi jela, Mandela alisema aliwasamehe maadui zake na kuwataka wananchi wa taifa hilo kushirikiana.
chanzo BBC
No comments:
Post a Comment