Wednesday, May 15, 2013

HIKI NDO KIASI ALICHOINGIZA MWANA FA KWA KUUZA RBT, KWELI HIP HOP INAUZA

Somebody please tell Madee kuwa hip hop inauza. Kwa mujibu wa Mwana FA mwenyewe ambaye leo ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.
IMG_1042
Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.
Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.
 chanzobongoclantblog

No comments:

Post a Comment