TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA.
wilaya ya chunya - kupatikana na
pombe haramu ya moshi [gongo].
mnamo tarehe 20.06.2013 majira ya saa
10:30hrs huko kijiji cha kamficheni- kasanga wilaya ya chunya mkoa wa mbeya.
askari polisi wakiwa katika doria/misako
walimkamata peter s/o malema, miaka 28, msafwa, mkulima, mkazi wa kijiji
cha kasanga akiwa na pombe haramu ya
moshi[gongo] yenye ujazo wa lita 5 ndani
ya nyumba yake. mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hiyo taratibu zinafanywa ili
afikishwe mahakamani. kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa
polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia pombe haramu ya
moshi[gongo] kwani ni kinyume cha sheria
na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
wilaya ya kyela - kuingia nchini bila
kibali.
mnamo tarehe 20.06.2013 majira ya saa
12:00hrs huko kasumulu wilaya ya kyela mkoa wa mbeya. askari polisi wakiwa katika doria/misako walimkamata akili s/o salim, miaka 25, mhutu,
raia na mkazi wa kongo akiwa ameingia nchini bila kibali. mbinu ni kusafiri kwa
njia ya kificho. taratibu zinafanywa ili
akabidhiwe idara ya uhamiaji. kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi
wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kuendelea kutoa taarifa katika
mamlaka husika kuhusu mtu/watu wanaowatilia shaka ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe
ikiwa ni pamoja na raia wa kigeni..
CHANZO http://habaribattle.blogspot.com
No comments:
Post a Comment