Mbunge wa arusha mjini Mh,Godbless Lema leo amefikishwa katika mahakama kuu kanda ya arusha
Mbunge
wa arusha mjini Mh,Godbless Lema leo amefikishwa katika mahakama kuu
kanda ya arusha kwa kosa linalomkabili lakutoa maneno ya ushoshezi kwa
mkuu wa mkoa arusha,tukio lililo tokeamnamo tarehe 24 mwezi wa nne
katika chuo cha uhasibu njiro.ambapo wanafunzi hao walikuwa
wamekusanyika katika eneo hilo wakitaka kuonana mkuu wa mkoa pamoja na
RPC ili kuzungumzia usalama chuoni hapo.
Akisomewa
shitaka hilo mahakamani hapo ,wakili wa serikali bi. Elianeny njiro
amesema mstakiwa lema alifika chuoni hapo siku ya tukio na kuongea
maneno kwa kutumia lugha ya uchochezi kwamba 'amekuja kama anakwenda
kwenye sendoff kauli hiyo
ilichochea vurugu kwa wanafunzi kwa kupelekea wanafunzi hao kurusha
mawe, chupa, wakati huo mkuu wa mkoa alipokuwa akitoa hotuba ,hali hiyo
ilipelekea uvunjifu wa amani.
Aidha
tukio hilo linatokana na mauaji ya mwanafunazi Henry Koga aliyefariki
23/4 kwa kuchomwa kisu na watu wasiofahamika na liliripotiwa polisi
ambapo polisi waliweza kufika eneo la tukio kwa na kufanya upelelezi
upelelezi ambapo upelezi huo uliendelea na mshtakiwa kufikishwa
mahakamani
katika
maelezo hayo wakili wa mshtakiwa bwana Method Kimomogoro alisema
maelezo yanayokubalika na kwamba mshtakiwa tarehe 24/4/2013 alikuwepo
chuoni hapo lakini maneno yaliyosalia kwamba alitoa maneno ya uchochezi
sio ya kweli.
Hakimu
aliyeendesha kesi Bi Devota Msofe alisema shauri la kesi hiyo litatajwa
kwa siku tatu mfululizo ambazo ni tarehe 20,21,22 mwezi wa nane huku
kukiwa na mashahidi kwa upande wa serikali ambao ni SSP Gilles
Muloto wa polisi arusha, Inspecta Jane mkaguzi wa polisi arusha
,inspeta Benard nyambanya,PC Godfrey johachimu Wiliamu mahanyi wa
polisi, Faraji kasidi wa chuo cha uhasibu njiro ,John Joseph wa chuo
cha uhasibu njiro,Benjamini simkanga wa chuo, na naibu hamidu,
No comments:
Post a Comment