Picha: Beyonce aendelea kuutukuza utamaduni wa kitanzania
Hivi karibuni mama Blue Ivy Beyonce Knowles kutoka Marekani alionekana katika moja ya show zake za Mrs Carter World tour akiwa amevaa vazi la kanga
lenye maneno ya kiswahili “Wawili Ninyi Yawahusu….”
ambalo
lilitengenezwa na mwanamitindo mtanzania Christine Mhando aishiye
Uingereza. www.shaddyclassic.blogspot.com
Beyonce ameendelea kuvaa vitu vyenye asili ya Africa baada ya kupiga
picha za jarida la Flaunt akiwa amevaa urembo wa Kiafrika ambao
huvaliwa zaidi na watu wa kabila la kimasai hapa Tanzania.
Picha hizi za Beyonce akiwa amevaa kiafrika zilipigwa mwaka 2011 lakini haijulikani kwanini amekuja kuzitumia wakati huu.
No comments:
Post a Comment