AMREF TANZANIA NA MONTAGE LIMITED WAANDAA CHAKULA CHA HISANI
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Montage Limited Bi Teddy Mapunda akitoa shukrani kwa Wadhamini na
wahisani waliojitokeza katika Kushiriki nae kuandaa Hafla ya Usiku wa
Chakula cha Hisani uliofanyika Jana katika Hotel Ya Serena ikiwa na
Lengo na kutafuta pesa kwaajili ya Kusomesha Wakunga ili kuweza kusaidia
katika kupata wakunga ambao Watatoa huduma na kupunga Vifo vya Mama na
Mtoto hafla hiyo iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na
Montage Limited na Bank kupitia Kampeni ya AMREF iitwayo Stand Up for
Tanzania Mother iliyozinduliwa mnamo tarehe 15 Mei 2013.
Mwenyekiti wa Benki M ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Musoma Mh Nimrodi Mkono Akitoa neno kwa wageni
waalikwa katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani kwaajili ya
kuchangisha pesa ya kusomesha wakunga, Hafla iliyofanyika katika Hoteli
ya Serena Jana Usiku Huku ikiwa imeandaliwa na AMREF Tanzania kwa
kushirikiana na Montage na Benki M kupitia Kampeni ijulikanayo Stand Up
for Tanzania Mothers
Mmoja wa Wanafunzi wa Masomo ya
Ukunga Kutoka Katika Jamii ya Wafugaji kutoka Kilindi Bi Tanioi Moringe
Akitoa shukrani zake za dhati Kwa AMREF Tanzania ambao ndio Wameweza
kumdhamini Kumsomesha Katika Chuo Cha Ukunga.
Makamu wa Raisi Mh Dk Mohamed Gharib
Bilal ambae pia alikua Mgeni rasmi katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha
Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage
Limited na Benki M akipokea mfano wa Hundi yenye Thamani ya Shilingi
Milioni 25 za Kitanzania kutoka Kwa Mwakilishi wa Benki ya NBC kwaajili
ya MChango wao katika Kampeni ya Stand up For Tanzania Mother ambayo
inalengo la kukusanya pesa kwaajili ya Kusomesha wakunga ili kusaidia
kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto
Mgeni Rasmi Ambaye pia Ni Makamu wa
Raisi Wa Tanzania Mh Dk Mohamedi Gharib Bilal akitoa Vyeti vya kushukuru
kwa wawakilishi wa Makampuni yaliyoweza kudhamini usiku huo wa Chakula
cha Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage
Limited na Benki M hafla iliyofanyika jana Usiku katika Hotel ya Serena
Baadhi ya Wawakilishi wa Makampuni
yaliyoweza kudhamini Hafla ya Usiku wa Chakula Cha Hisani ulioandaliwa
na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benk M
wakipokea vyeti vya Shukrani kutoka Mgeni Rasmi Dk Mohamed Gharib Bilal
ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jana
katika Hotel ya Serena.
Wadau waliohudhuria hafla ya Usiku
wa Chakula Cha Hisani wakiangalia jiwe la Tanzanite lililokuwa
likinadaiwa jana katika Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena
Wadau wakipata Msosi katika Hafla ya Usiku wa Chakula Cha Hisani uliofanyika jana katika Hotel ya Serena na kuandaliwa na AMREF Tanzania kwa Kushirikiana na Montage Limited na Benki M.
CHANZOhttp://jamiiblog.co.tz/
No comments:
Post a Comment