HISTORIA YA HAYATI BABA WA TAIFA MWL. JULIUS NYERERE (NYERERE DAY)
Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa
Butiama mkoani Mara mnamo tarehe 13 April 1922 na alifariki dunia 14
Oktoba 1999.
Alikuwa mojawapo
kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka
12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza
shule ya msingi aliendelea kusom
a
shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20
alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Mapadre
wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala,
Uganda kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa
wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African
Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora
akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda
kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma
M.A. ya historia na uchumi(alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika
chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya
juu nje ya Tanzania).
Aliporejea
Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na
Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.
Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African
Association (TAA), cham
a ambacho
alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha
Makerere. Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama
cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha
kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa
tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.
Uwezo
wa mwl. Nyerere uliwashitua uongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere
kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema
kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.
Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa
kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia
alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth
committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa
kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata
uhuru bila umwagaji wa damu.

Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana
Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere
aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri
mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe
9/12/1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na
mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya
Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya
Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid
bin Abdullah.
Sifa zake
Bado
anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake
za kujali utu na ubinadamu.Pia ataendelea kukumbukwa na waafrika kote
barani hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania
uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.
Mwishoni
mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake
Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) na kufariki Uingereza
wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba, 1999. Alizikwa
mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.

(Kaburi la Baba wa Taifa)
Watanzania
tumempoteza kiongozi mpiganaji na mwenye uchungu na nchi yake,
aliepinga vita dhidi ya umasikini, ubaguzi na rushwa. Hamna kiongozi
mwengine alieiga mfano wa Baba wa Taifa tumebakiwa na viongozi wenye
uchu na madaraka kujirumbukizia mali wao na familia zako ni aibu sana
kwa Taifa maana enzi za Mwalimu hapakukuwa na hali hii ya kiongozi
kumiliki mali nyingi mfano mzuri alionesha yeye ambae hakuwa na uchu wa
kujirumbikizia mali ingawa alikuwa na nafasi kubwa na inayomfanya aweze
kufanya hivyo lakini alikuwa na uzalendo na nchi yake. Nchi sasa
inapoteza dira hamna viongozi bora ila kuna bora viongozi aibu kwa
Watanzania.
No comments:
Post a Comment