Sunday, October 13, 2013

UFOO SARO AFANYIWA UPASUAJI MUHIMBILI NA KISA KIZIMA CHA UNYAMA HUO.

Mtangazaji wa ITV na Radio One, Ufoo Saro amefanyiwa upasuaji baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi na mzazi mwenziye aitwaye Anther Mushi mapema leo.

 Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni. 


Ufoo alipigwa risasi akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi Annastazia Saro baada ya kutokea mgogoro baina yake na mzazi mwenziye.



Katika tukio hilo, Anther alimpiga risasi na kumuua mama Ufoo kisha na yeye akajilipua kwa risasi baada ya kumpiga risasi Ufoo.
 
Baadhi ya waandishi na wananchi wakiwa wamekusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujua hali ya Ufoo.
 
 Kwa sasa Ufoo amehamishiwa katika wodi ya Kibasila anapoendelea kupatiwa matibabu. 

Umati wa watu ulikusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi ili kujua hali ya mtangazaji huyo.

Pichani chini baadhi ya Wafanyakazi wenzake na Ufo Saro kutoka IPP pamoja waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Wafanyakazi hao wakibadilishana mawazo hapa na pale katika hospitali ya Muhimbili leo hii 

 Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro,  baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake  Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mtu aliyedaiwa ni mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua.
 Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati 
CHANZO http://paparaziblog.blogspot.com

No comments:

Post a Comment