MAMA WA UFOO SARO AZIKWA MACHAME
Mtoto
wa mwandishi na mtangazaji wa kituo cha ITV,Ufoo Saro,Alvis Anthery
akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la marehemu Bibi yake Anastazia
Saro aliyezuikwa jana katika makaburi ya kanisa la Urara wilayani Hai.
Umati
wa waombolezaji waliojitikeza katika kuaga mwili wa marehemu Anastazia
Saro aliyezikwa katika makaburi ya kanisa la Urara wilayani Hai.
Msemaji wa familia ya Saro,Allelio Swai akitoa maelezo ya familia wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Anastazia Saro.
Mkuu
wa jimbo la Hai,Aminirabi Swai akiongoza ibada ya maziko katika
makaburi ya kanisa hilo na kisha kuweka shada la maua katika kaburi la
marehemu Anastazia Saro.
mwakilishi
wa serikali katika maziko ya marehemu Anastazia Saro ,mkuu wa wilaya ya
Hai Novatus Makunga akiweka shada la Maua katika kaburi.
Mtoto Alvis Anthery akiweka shada la maua katika kaburi la Bibi yake marehemu Anastazia Saro.(picha na Dixon Busagaga)
Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi
VILIO,simanzi
na hali ya huzuni jana vimetawala kwa mamia ya wakazi wa kijiji cha
Shari, Machame wilayani Hai waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu
,Anastazia Saro (56),mama mzazi wa Mwanadishi na Mtangazaji wa Kituo cha
Televisheni cha ITV,Ufoo Saro.
Wakazi
hao wakiwemo wale waliotoka maeneo mbalimbali ya miji ya Moshi,Arusha
na Dar es Salaam baadhi yao walionekana wakiangua vilio huku wengine
wakipoteza fahamu muda mfupi baada ya jeneza lililobeba mwili wa
marehemu kuingizwa kanisani.
Hali
ilikuwa ya Simanzi zaidi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa
waombolezaji wakipita mbele ya jeneza ambapo ililazimika kuwepo na watu
maalumu ambao walikuwa na jukumu la kutoa huduma ya kwanza kwa baadhi ya
ndugu walioshindwa kujuzuia.
Hali
kama hiyo ili rejea kwa mara nyingine tena pale msemaji wa familia
Allelio Swai akitoa maelezo ya namna marehemu alivyo uawa na hali
aliyokutwa nayo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari.
Akitoa
maelezo ya wasifu wa marehemu aliyefanyiwa ibada ya mazishi katika
Kanisa la Urara lililopo chini ya Jimbo la Hai la Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT),Swai alisema marehemu Anastazia Saro alifikwa
na mauti hayo baada ya kupigwa risasi na mkwewe Anthery Mushi ambaye
alikwenda nyumbani kwa mama huyo eneo la Kibamba CCM,nje kidogo ya Jiji
la Dar es Salaam.
Alisema
taarifa ya madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),
inaonyesha,Anastazia Saro alifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa
risasi tano katika mwili wake.
Swai
aliomba kufanyika maombi kwa ajili ya Ufoo aliyelazwa katika hosptali
ya Muhimbili ambako anapatiwa matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji
mkubwa hali iliyolazimu madaktari kumpa muda mrefu wa mapumziko.
“
Ufoo taarifa ya madaktari inaonesha alichanika utumbo mkubwa na kiasi
utumbo mdogo,lakini tunashukuru hali ya Ufoo inaendelea kuimarika
,lakini maombi yenu yanahitajika ili aweze kurejea katika hali yake ya
zamani ,na aweze kulitumikia taifa kwa kuhabarisha “alisema Swai.
Kwa
upande wake,baba mdogo wa Ufoo Saro, mzee Eshikaeli Saro, akizungumza
katika ibada ya mazishi kanisani hapo,alisema familia na kanisa
imepoteza mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya jamii na kanisa.
“Mama
alikuwa ndiye mpambaji wa madhabahu ya kanisa ,na alihakikisha kanisa
linakuwa katika hali ya usafi kabla ya ibada na hata pale wanakwaya
walipokuwa na mazoezi ya kutwa hapa kanisani alihakikisha wanapata
chakula”alisema Saro.
Alitoa
shukrani kwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Dk.Regnald
Mengi,mkurugenzi mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile pamoja na
wafanyakazi wote wa makampuni hayo kwa kuifanya familia hiyo iweze
kumfikisha marehemu Machame na kuzikwa.
Marehemu
Anastazia Saro, aliuawa baada ya mkwewe kufika nyumbani kwake Kibamba
CCM akiwa na mzazi mwenzie Ufoo kwa lengo la kusuluhishwa kile
kinachodaiwa ni ugomvi uliokuwa ukifukuta kati ya wawili hao.
Tukio
hilo lilitokea alfajiri ya Jumapili ya Oktoba 13 mwaka huu, huku mwanae
Ufoo Saro ambaye ni Mwandishi na Mtangazaji wa ITV, akijeruhiwa vibaya
kwa risasi mbili baada ya kutokea ugomvi kati yakena mzazi mwenzie
Anthery Mushi ambaye hata hivyo na yeye alijiua kwa kujipiga risasi
baada ya tukio hilo.
chanzo:michuzi matukio
No comments:
Post a Comment