Membe amlipua Wenje
Dodoma. Wakati
Bunge likipitisha bajeti ya makadirio ya matumizi Sh191.91 bilioni ya
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha
2014/15 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard
Membe, alitumia nafasi hiyo ‘kumchana’ Ezekiel Wenje na kusema kuwa
anatumiwa na mataifa ya nje.
Mbali na hivyo aliwaita watu
wanaotoa kauli za uchonganishi kuwa ni wapumbavu na akataka waache tabia
za kipumbavu kwani hawatavumiliwa hata kidogo.
Membe alitoa kauli hiyo jana jioni wakati akitoa majumuisho katika
michango ya wabunge kwenye hotuba ya mapato na makadirio ya wizara hiyo
kwa mwaka 2014/15.
Wenje ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa jana asubuhi katika hotuba yake, alimshambulia
Membe kuwa ni waziri mzigo ambaye hajui wajibu wake.
Sakata hilo liliibuliwa kwenye uhusiano baina ya Tanzania na nchi ya Rwanda ambalo Wenje alilizungumzia zaidi.
Akijibu hoja hizo Membe, alisema: “Kwanza nikubaliane na kauli ya
wabunge wengi kuwa uhusiano wa Tanzania na Rwanda siyo mzuri kwani kila
upande haumuamini mwenzake,” aliema Membe.
Alisema kinachowaumiza pande zote ni kuwa kila upande unapozungumza
na mahasimu wa mwenzake, wanahisi kuwa anataka kuipindua Serikali yao
hivyo bado hawajakubaliana kwa jambo lolote lakini akasema yote
yatakwisha salama.
“Huwezi kusimama hapa mtu na macho yakakutoka halafu unaanza
kulizungumzia taifa lingine ambalo siyo lako, hivi unatoa wapi ujasiri
huo au wanakulipa,”alihoji Membe na kuongeza.
“..Mimi naweka rehani uwaziri wangu hapa kwamba ukileta vielelezo
kamili mimi nitakuwa tayari kuachia nafasi yangu, je na wewe nikitoa
vielelezo utakuwa tayari kuwajibika.”
Alimtaja Wenje kwa jina kuwa alichokifanya hakifai kuwa alitoa kauli
ambayo siyo nzuri kwa siri za taifa na akasema mtu kama huyo akipata
nafasi hata kama nchi itakuwa vitani, yuko tayari kutoa siri.
Aliyataja makundi ya ya M23 kuwa ni moja ya kundi ambalo linaundwa na
Banyamulenge waliokuwa chini ya Roral Nkunda pamoja na kundi la FDRA
ambalo liliua watu wengi kwamba linaundwa na Wahutu bila ya ubishi.
Membe alimpongeza mbunge Alli Keissy kuwa alichokizungumza jana
asubuhi kuhusu Rwanda na DRC Kongo ni sahihi na ndiyo maana
alimshangilia kwa nguvu zote.
No comments:
Post a Comment