ADAU WA SEKTA YA MAWASILIANO WAKUTANA ARUSHA
Mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Kenya
Mkurugenzi mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Uganda Patrick Mwesigwa
Mkurugenzi wa Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema
Balozi Joseph Bangurambona wa Burundi akiongea juu ya mkutano huo
Wadau wakifatilia mkutano leo jijini Arusha
Kulia Pamela Mollel wa jamiiblog na Jusline Marcko wa gazeti la Siha Leo
Wadau zaidi
ya mia moja kutoka taasisi za mamlaka ya mawasiliano Afrika Mashariki
(EACO} wamekutana jijini Arusha ili kuangalia namna ya kuweza kutatua
changamoto zilizopo katika sekta hiyo muhimu ya mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Kenya alisema kuwa mkutano huo unalenga kujadili changamoto zilizobainishwa na wadau wa sekta hiyo kuhusu vikwazo ambavyo vinakwamisha mbalimbali usambazaji wa mawasiliano kwa nchi hizo.
Wangusi alisema kuwa sekta
ya mawasiliano ina vitengo mbalimbali ikiwemo posta,mawasiliano ya simu
na utangazaji na mitandao ya kijamii(internet) ambayo bado inakabiliwa
na changamoto nyingi zinazohitaji juhudi za wadau wa sekta hiyo ili kuwafikia watumiaji.
Aidha alibainisha kuwa huduma ya posta bado inakabiliwa na changamoto ya anuani makazi ili kuwawezesha watumiaji wanaoutumia huduma hiyo iweze kuwafikia kwa haraka kama zilivyo huduma nyingine.
Hata
hivyo wangusi aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa ni mawasiliano
ya huduma za simu katika nchi za Afrika mashariki ambapo mbali na watoa
huduma kupata faida kubwa lakini pia wanawatoza watumiaji gharama kubwa
hivyo kupelekea watumiaji kutoka nchi moja hadi nyingine kushindwa
kumudu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Watumiaji
wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema
alisema lengo ni kuangalia kuwa mawasiliano yanawafikia watumiaji na kufaidi huduma hiyo ya simu,internet,utangazaji na maswala ya posta.
Alisema
kuwa mawasiliano hayafahamu mipaka hivyo ni wajibu wa watoa huduma
kutoa huduma bora na nafuu ili watumiaji waweze kuwasiliana na kuungana
pamoja katika maswala mbalimbali likiwemo swala la ukuaji wa uchumi.
Mkutano
huo umekutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano kutoka nchi tano
zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki lengo likiwa ni kutoa majibu ya
changamoto hizo ambapo mwenyeji wa mkutano huo ni Tanzania,
No comments:
Post a Comment