Watu watatu wakazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam wamejeruhiwa
katika tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na
polisi baada ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma maarufu Kigodoro, ambazo
tayari zimekwishapigwa marufuku na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar
es Salaam.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na nusu jioni katika eneo la shule ya msingi kisiwani ambapo Star TV imetembeelea majeruhi
hao ambao mmoja tayari amekwisahruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine
akiendelea na matibabu kwenye hospitali ya Mwananyamala.
Wakiwa kwenye ngoma hiyo maarufu Jijini Dar es Salaam ya Kigodoro, eneo
la Kisiwani mwananyamala, mara gahfala polisi walivamia eneo hilo, na
kusimamisha shughuli nzima kwa madai ya kucheza wakiwa hawana nguo,
jambo ambalo ni kinyume na maadili.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanaelezea namna wakazi hao walivyojeruhiwa.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi
Kinondoni Kamishna msaidizi Camillius Wambura anathibitisha kutokea kwa
tukio hilo.
Hali za Majeruhi hawa zinaendelea vizuri na tayari wameruhusiwa kutoka hospitalin
No comments:
Post a Comment