Thursday, June 26, 2014

HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ILIYOTOLEWA NA UONGOZI WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
OFISI YA MKOA
S.L.P 345
SINGIDA
25/ 06 /2014.
TAARIFA RASMI YA CHAMA MKOA WA SINGIDA KUHUSU UPOTOSHAJI WA HABARI ZILIZOTOLEWA NA WATU WANAOJIITA VIONGOZI WA CHADEMA TOKA SINGIDA
Ndugu, waandishi wa habari kama ilivyotangazwa tarehe 23/06/2014 katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa kuna viongozi toka mkoa wa Singida kwa kujitangaza kuwa wao ni wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu Chadema Taifa , Taarifa hizo sio za kweli na ofisi ya chadema Mkoa wa Singida tunazikanusha taarifa hizo kwa nguvu zote na kuzitolea ufafanuzi kama ifuatavyo.
1. HAMIDA SUDI, JOSHUA MOYO.
Waliojitambusha kuwa wao ni viongozi wa mabaraza na wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu Taifa toka Singida, ukweli ni kwamba chadema haina viongozi hao katika ngazi zote za kata, jimbo, wilaya au Mkoa. Hao waliojitambulisha kwa majina hayo na nafasi hizo. Hivyo watu hao ni matapeli wa kisiasa na tunawaomba wananchi wa Singida na watanzania wawapuze na wasiwaamini maneno yao na utambulisho wao.
2. DOTO BARUANI :
Ndugu waandishi wa habari kuna jina DOTO BARUANI, huyu ni mwenyekiti wa chadema wilaya ya manyoni, watu hao wameorodhesha jina la mwenyekiti kuwa alihudhuria mkutano huo, ukweli mwenyekiti wetu siku ya tarehe 23/06/2014 alikuwa katika mikutano ya chama wilaya ya manyoni na bahati nzuri tuko nae hapa kwa sasa. Hapo / inaonekana na kujidhihirisha kuwa kuna watu wako tayari kutumia majina ya watu wengine kwa maslahi yao binafsi na tunaomba, wawajibishwe kisheria.
3. EMMANUEL KITUNDU
Ndugu waandishi wa habari huyu nikweli alikuwa kiongozi wa Bavicha wilaya Singida mjini kwa nafasi ya Mwenyekiti, Mtu huyu ukomo wake wa uongozi uliisha tarehe 08/03/2014 baada ya kuthibika kuwa amekuwa kibaraka wa chama cha mapinduzi ccm ndipo kamati ya utendaji wilaya ya Singida mjini ilipokaa tarehe hiyo na kumvua uongozi na uanachama. Hivyo kuendelea kijitambulisha kama kiongozi wa chadema na mwenyekiti wa M4C ni makosa. Hata hivyo kama angekuwa kiongozi kwa nafasi ya aliyojitambulisha asingekuwa mjumbe wa baraza la kuu wala mkutano mkuu Taifa, wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza kuu, kikatiba ni wenyeviti wa wilaya na Mikoa na makatibu wa ngazi za wilaya na mikoa ni wakaribishwa tu. Baada ya kuvuliwa uongozi kamati tendaji ilikaimisha ndugu KHALIKI MWAKA.
4. Kuhusu uchaguzi wa ndani ya chama hadi sasa unaendelea vizurikadri ya matakwa na maslahi ya chama kikilenga kukuimilikisha chama kwa watu kuanzia ngazi ya mashina. Maeneo mengine uchaguzi umeshafikia ngazi ya kata, majimbo na Wilaya. hatimae tutaelekea hadi mkutano mkuu na utatanguliwa na baraza kuu
5. Kuhusu matumizi ya rasilimali za chama chetu Chadema kimekuwa kikiongoza kwa kuwa wazi katika mapato na matumizi ikiwemo kuwasilisha mapato na matumizi kwa ofisi msajili wa vyama vya siasa kila mwaka ni uwazi huu katika mapato na matumizi ulimfanya mkaguzi na mthibiti mkuu wa mahesabu ya serikali (CAG) alipofanya ukaguzi kwenye chama chetu hakukuta tatizo wala ufisadi wowote hilo linathibitishwa naripoti ya CAG aliyoitoa mwaka huu.
6. Kuhusu vikao vya katiba ya chama suala hili liko wazi kwenye katiba ya chama mwaka 2006ambayo inaweka bayana kuwa baraza kuu litakutana kkila mwaka mara moja kwa kikao cha kawaida au kwa dharura. Mkutano mkuu unapaswa kufanyika kila baada ya miaka mitano, tulivyokutana kwenye kikao cha baraza kuu mwaka jana tarehe 28/01/2013 ukumbi wa Kareemjee Dar es salaam tulipanga vikao vya mwaka huu vya baraza kuu na mkutano mkuu hatuna tatizo na ratiba kwa sababu tunajua mwaka huu vikao vya kikatiba vitafanyika kwa mamlaka yetu ya kikatiba mwaka jana kikao cha baraza kuu kilikasimisha madaraka kwa kamati kuu na sekretarieti kusimamia ratiba hiyo kwa kadri ya matakwa na maslahi ya chama.
7. Katika kikao hicho cha baraza kuu la chama mwaka jana pia tuliazimia kuhusu mpango wa M4C kama sehemu ya uenezi na uhamasishaji wa chama na pia tukaazimia kuhusu matumizi ya chopa (Helkopta) katika mikakati ya uenezi na uhamasishaji wa chama ili kuwafikia wananchi wengi kwa haraka na wapiga kura kwenye chaguzi.
8. Suala la chama kumiliki ofisi zake hadi sasa tuna maeneo ambayo chama kinamiliki majengo na hati za umiliki wa ardhi. Hii ni tofauti na ccm ambayo hadi leo haina majengo wala ardhi yake yenye zaidi mali za wananchi wote.
Ndugu waandishi wa habari mtakumbuka tarehe 3/ 12/ 2013 mlitwa na mtu aliyejiita yeye ni mwasisi wa chadema mkoa wa Singida, sina haja ya kumtaja jina lake, mtu huyu alitangazia dunia kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama kwa sababu alizozitaja na sisi chadema Mkoa tulitoa taarifa ya kumvua uanachama rasmi mwezi moja baadae, cha ajabu tena anaibuka na kudai yeye ni kiongozi na mjumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu Taifa toka mkoa wa Singida.
Mtu huyo ni mwongo mpotoshaji na mbabaishaji katika siasa tunawaomba watanzania na wanasingida na wanachama wampuuze na wasiendelee kumpa ushirikiano kwa niaba ya chadema.
MWISHO:
Sisi viongozi wa chadema Mkoa wa Singida tunawathibitishia wananchama wetu wapenzi na wananchi wote kwa ujumla wake tuko imara hatujaterereka, hatutatetereka na propaganda za waongo, walioshindwa siasa, sisi tuko imara tnasonga mbele mpaka kieleweke.
Tamko hili limetolewa na baraza la uongozi la mkoa wa singida.
Imeandaliwa Na Baraza La Chadema Mkoa Wa Singida
…………………………………
SHABANI LYIMU
M/KITI CHADEMA
MKOA WA SINGIDA.

No comments:

Post a Comment