Leo ni siku yanne tangu katibu wa Chadema mkoa wa Tabora kwa niaba
ya wajumbe 78 wa baraza kuu na viongozi wengine wa mabaraza ya vijana na
wanawake 4 na kufanya kuwa jumla ya wajumbe 82 kwa pamoja kuzungumzia
maswala mbali mbali waliyosema yanatishia ustawi wa chadema leo wameenda
kwa msajiri wa vyama pamoja na mkaguzi wa mahesabu ya serikali CAG.
Mapema
leo wamekwenda kwenye ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa na kukabidhi
barua yenye malalaiko mbali mbali juu ya walichokisema kuwa uvunjifu ya
katiba unaofanywa kwa makusudi na viongozi wa chadema ambaye ni
mwenyekiti mbowe na katibu mkuu slaa. Tunaambatanisha na nakala ya barua
tuliyoipeleka kwa msajiri.
Ingawa
walifanikiwa kuzifikisha barua hizo sehemu zote mbili licha ya kikwazo
ambacho kiliwekwa na jeshi la polisi kwenye ofisi ya mkaguzi wa mahesabu
ya serikali baada ya kuonekana wamepeleka barua hizo kwa maandamo na
mabango.
Chini ya hizi picha nimeambatanisha barua zote mtu wangu wa nguvu,nilipozipata nimeona nikuwekee na wewe usome.
Hii ni barua iliyopelekwa kwa CAG
JORUM ABDALLAH MBOGO
S.L.P 1110
TABORA
25.06.2014
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI
MTAA WA SAMORA NA OHIO
S.L.P 9080
DAR ES SALAAM
+255(22)2115157/8
DAR ES SALAAM.
YAH: MAOMBI YA TAARIFA YA UKAGUZI WA CHADEMA.
Husika na somo hapo juu.
Mimi ni mwanachama na kiongozi wa ngazi ya wilaya wa Chama cha
Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la
chama
Kwa kipindi kirefu ndani ya chama chetu tumekuwa tukilalamikia
matumizi mabaya ya pesa hasa za ruzuku, pesa ambazo msingi wake ni kodi
za wananchi na hivyo kuwa ni pesa za umma. Hii inatokana na ukweli
kwamba mpaka sasa chama kimepokea jumla ya BILION 10.038 kama ruzuku kutoka serikali kuu, kwa kipindi cha miezi 42 kutokea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Tumejitahidi sana kudai taarifa sahihi za matumizi ya pesa hizo bila mafanikio.
Kwa kuwa tunatambua kwamba ni hivi karibuni tu, ofisi yako imemaliza kufanya UKAGUZI MAALUM WA MAHESABU KWA VYAMA VYA SIASA kikiwemo na CHADEMA, na kwamba taarifa yake mmeshaiwasilisha Bungeni.
Kutokana na ukweli kwamba wengi wetu sisi sio wabunge na hatuna uwezo wa kuipata hiyo Taarifa ambayo ni muhimu sana.
Na kwa kuzingatia kwamba sisi ndio wenye chama na sisi ndio walipa
kodi zinazoipatia chama Ruzuku. Ni wajibu wetu kusimamia matumizi yake.
Hivyo basi, kwa niaba ya viongozi na wanachama wenzangu wasiopungua 82, tunaiomba ofisi yako itusaidie yafuatayo
- ITUPATIE NAKALA YA TAARIFA ILIYOKAGULIWA
- IITOE NAKALA HIYO KWA UMMA ILI UMMA UJUE NAMNA KODI ZAO ZINAVYOTUMIWA
Tunatumaini kwamba Ombi letu litashuhulikiwa kwa uzito na umuhimu wa kipekee
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
Wako katika ujenzi wa Taifa
……………………………………………………
JORUM ABDALLAH MBOGO
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Hii ni barua iliyopelekwa kwa msajiri wa vyama vya siasa.
JORUM ABDALLAH MBOGO
S.L.P 1110
TABORA
25.06.2014
MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
S.L.P 63010
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Ndugu,
YAH: MAOMBI YA UFAFANUZI WA KIKATIBA JUU YA UVUNJIFU WA KATIBA NA YA CHAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI
Mheshimwa Msajiri, Somo hapo juu la husika.
Mimi ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,
Kwa niaba ya wanachama wenzangu, tunaleta kwako malalamiko ya
uvunjifu wa katiba ya chama Yanayotokana na matamko yanayoendelea
kutolewa na viongozi wa kitaifa juu ya kuungana na UKAWA yenye tafsiri
kwamba wataachiana majimbo ya kugombea ili waweze kuingia madarakani na
kuunda serikali ya pamoja.
kama hivyo ndivyo wanakiuka SURA YA TISA. IBARA YA 9.3.1 ya KATIBA YA CHADEMA inayosema ‘’chama
kinaweza kuunda mseto na chama au vyama vingine vyenye madhumuni na
malengo yanayofannaili kuimarisha iwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au wa
serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja’’
Kwa kuwa viongozi wa CHADEMA na CUF na NCCR wameungana na kuunda
chama kingine cha UKAWA kwa mujibu wa SURA YA TISA ibara ya 9.3.3 ‘’chama kinaweza kuungana na chama ama vyama vingine kuunda chama kipya’’ hivyo wamevunja SURA TISA, Ibara ya 9.3.4 inayosema ‘’Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1, na 9.3.3 utafanywa na mkutano mkuu wa Taifa na kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza KUU’’.
Na hivyo sisi kama chama hatujakaa BARAZA KUU ili kupitisha AGENDA za
huo mkutano mkuu na wala MKUTANO mkuu haujaitishwa kujadili maamuzi
hayo yaliyofikiwa na viongozi wetu.
Mheshimiwa Msajiri, Tunafahamu kwamba KANUNI za chama SURA YA TISA
kuanzia ibara ya 9.0 Mpaka ibara ya 9.7 zinatoa uhuru wa chama kuungana
na kufanya ushirika na vyama vingine kwa kadri itakavyoona inafaa.
Ila kanuni hizi zinaweka mkanganyiko wa kitafsiri, na hivyo zinazuiwa na kuuliwa nguvu na Ibara ya 9.2.3 ya KATIBA YA CHAMA Inayosema ‘’kukitokea migongano kati ya kipengele cha katiba na kile cha kanuni, kipengele cha katiba kitatawala’’. Hivyo kanuni zinazotoa uhuru huo haziwezi kutumika hapa.
Mheshimiwa msajiri, kwa kuwa wewe ndio mlezi na msimamizi wa vyama
vyote vya siasa, na kwa kuwa hakuna chama cha siasa kilicho juu ya
katiba yake, hivyo tunakuomba uingilie kati mgogoro huu wa uvunjifu wa
katiba unaofanywa kwa makusudi na viongozi wa chama.
Tunakuomba pia uuagize uongozi wa kitaifa uitishe haraka kikao cha
baraza kuu, kwani tumeshapitisha miezi mi nne sasa ya kisheria ambayo
baraza kuu lilipaswa kukaliwa, mara ya mwisho tulikaa kikao cha baraza
kuu mwezi febryary mwaka 2013, hivyo tulitakiwa tena tukae baraza kuu
mwezi February mwaka huu. Hatujaitwa, wala hatujapewa sababu yoyote
yenye mantiki.
Vile vile tunakuomba uwaagize viongozi wa chama waitishe chaguzi
halali za zhama na waache kuchomeka watu wao wanaowataka kwa hila, kwa
mujibu wa ratiba tulizozipitisha uchaguzi ulupiswa kuwa umeshafanyika
kufikia December 2013, na baadae june 2014, lakini mpaka
tunavyokuandikia leo, hakuna lililofanyika.
Tunakutakia kila la heri katika kutusaidia ufafanuzi huu.
Tunatanguliza shukrani za dhati na tukiamini swala letu litafanyiwa linavyostahili.
Wako katika ujenzi wa Taifa.
JORUM ABDALLAH MBOGO
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA
No comments:
Post a Comment