NCHEMBA ASEMA ATAONGOZA MAPAMANO YA KUMNG'OA MSIGWA
Naibu katibu mkuu wa CCM bara Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini.
Wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza Nchemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa.
Na Francis Godwin Blog
NAIBU katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bara Mwigulu Nchemba
awahakikishia wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa muda wa mbunge
wa jimbo hilo kuongoza umefika kikomo na kuwa ataongoza mapambano ya
kumng’oa mwakani katika uchaguzi mkuu.
Akiwahutubia
wananchi wa jimbo la Iringa mjini leo katika uwanja wa Mwembetogwa
Nchemba ambae ni naibu waziri wa fedha alisema kuwa mbali ya mbunge
huyo kupewa nafasi hiyo ya bure mwaka 2010 ila bado ameshindwa kuwa na
huruma na wananchi wa jimbo hilo na kuendelea kujinufaisha yeye badala
ya kuwekeza kwa wananchi hasa vijana na ndio sababu ya kushindwa
kufanya vikao na wanachama wake na kuendelea kuitisha maandamano badala
ya kufanya kazi.
“Tutajipanga
vema kila kona ya jimbo la Iringa mjini ili kulirudisha jimbo mikononi
mwa CCM kwa kumpata mbunge ambae atawatumikia wananchi na sio wa
kujitumikia yeye na kuwa mbunge wa maandamano kwa kipindi chake chote”
Nchemba
alisema kuwa kutokana na kazi kubwa iliyopfanywa na vijana wa jimbo la
Iringa kwa kumpigania mbunge Msigwa alipaswa kuwa na roho ya huruma
kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kuwageuza daraja na kuwafanyisha
maandamano yasiyo kwisha badala ya kuwaanzishia miradi ya kiuchumi.
“Hivi
tazameni leo maeneo yote ya makanda wa Chadema majimboni mwao ni
maandamano kila siku kila wakati utasikia hakuna kulala makamanda huku
mbunge anashindwa kuwasaidia …..na siku hizi wanakuja na hoja ya
makamanda pambaneni tutachukua nchi huku hata kata kwao ni ndoto sasa
niwaambie leo hata nusu ya nchi hii kamwe hawatapata”
Asema
mmoja kati ya mke wa kiongozi mojawapo wa Chadema alimuuliza hivi kwa
nini mume wake anapenda sana maandamano alimjibu kuwa mume wake huyo
akichukia huwa anafanya maandamano ndani ya chumba cha kulala.
Nchemba
pia ameponmgeza utendaji kazi wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
Ritta Kabati na kuwa siku zote amekuwa akiwapigania wananchi wa jimbo
la Iringa mjini bungeni tofauti na mbunge wa jimbo mchungaji Msigwa
ambae amekuwa akiongoza kwa kufanya maandamano.
Katika
hatua nyingine Nchemba alisema amesema kuwa muda wa matajiri
kuendelea kujinufaisha na misamaha ya kodi umekwisha na kuwa
anajipanga kupeleka sheria bungeni itakayowabana wafanyabiashara
wakubwa kulipa kodi kama wanavyolipa wafanyabiashara wadogo.
Alisema
kuwa watu wanapata misamaha hadi inakatisha tamaa kwani ni pesa
nyingi za kimaendeleo zinapotea kutokana na utitiri wa misamaha
inayoendelea kutolewa .
“Napeleka
sheria katika bunge hili la bajeti itakayofuta misamaha ya kodi kwa
viwanda na wafanyabiashara wakubwa…inakuweje wananchi masikiti hata
wanapotaka kuanzisha saluni wanalipizwa kodi ila wafanyabiashara
wakubwa na baadhi ya watu pia nitapeleka sheria ya kubana matumizi ya
fedha za umma”
Alisema
kuwa inashangaza kuona mashirika ya umma yanavuna na kutumia huku
wanyonge wakiendelea kuteseka na walimu na askari wakiendelea kukosa
kulipwa madai yao.
“hatuwezi
kusema leo walimu ama askari ni wengi wakati watu wanakwepa
kulipa kodi huku wanafunzi wakikosa mikopo ya elimu ya juu eti
kutokana na kukosa fedha wakati watu wengine wanakwepa kodi….hili ni
jambo la aibu sana najua wapo wabunge watakaopinga ila wananchi
mtaona ni nani ni mbunge wa wananchi …kwani najua wapo wabunge ambao
hawalipendi hili watapinga ila lazima nilifikishe hata kama chungu ila
lazima suala hili likomeshwe”
No comments:
Post a Comment