Saturday, June 21, 2014








magessa





Katika picha ni Bw.Joseph Magessa aliyetuhumiwa hivi karibuni na tukio la Nyoka aina ya Chatu.
 
 
 
 
 
 
 
 
SAKATA la kukutwa na chatu  eneo la sakina katika nyumba ya Joseph Magessa limechukua sura mpya baada ya  mhusika kuhojiwa na mtandao huu wa jamiiblog kuhusiana na tukio hilo.
 
Aidha chatu huyo ambaye alikutwa  nyumbani kwa mmiliki huyo hivi karibuni imeelezwa tuhuma hizo sio za kweli bali ni njama za kumwaribia tu na tukio hilo ni la kutengenezwa na watu kwa lengo la kumchafulia jina lake.
 
Magessa alisema kuwa ,ameshangazwa sana na tukio hilo kwani lilipotokea alikuwa safarini yeye na mke wake , ndipo alipopigiwa simu kuhusiana na tukio hilo na kuwataarifu  huyo chatu auawe.
.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu  zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Aliongeza kuwa, yeye hajawahi kuwa mshirikina wala mke wake bali wanachojua wao ni kuwa wanamtumikia Mungu na yeye pekee ndiye ajuaye kila jambo na kuwa mambo yote hayo yaliyotokea amemwachia Mungu ndiye atakayejibu.
Magessa alifafanua kuwa, ameshangazwa sana na  taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikizushwa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao juu ya tukio hilo ila yeye amenyamaza kimya na amemwachia mungu kwani ndiye ajuaye kila kitu.
KUHUSU KUTENGWA KWAKE  KANISANI .
Aidha akizungumzia kuhusiana na swala la kutengwa kwake na Kanisa katoliki alisema kuwa huo ni uongo na uzushi hakuna kitu kama hicho kwani wanamwelewa vizuri sana tabia yake na kuwa hana tabia ya ushirikina.
‘Tena waumini wa kanisa katoliki watakuja kufanya jumuiya nyumbani kwangu na tayari kuna masalaba pale kama kweli ningekuwa nimefanya hivyo leo hii wangefuata nini hapa kanisani’alisema Magessa.
 Naye mkewe Selina Magessa , akizungumza na jamiiblog kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa.tangu ameanza kuishi na mumewe miaka mingi hadi sasa hivi ,hajawahi kusikia wala kuona
vitendo vya ushirikina.

“Niko na mume wangu miaka mingi, sijawahi kusikia kuwa anafuga nyoka ndani wala sijafiwa na mtoto yeyote, wote watatu wapo ila nashangaa kusikia kauli kwamba mume wangu aliagiza nyoka asiuawe kwa kuwa ni mtoto wake ama mama yake mzazi,” alisema Selina.

Alisema kuwa , kwa sasa hivi ni muda wao kupumzika na kutafakari mambo yao sio wakati wa kuzungumzia swala hilo tena kwani wamechishwa na maneno kila mahali ili wanachofanya ni kumwachia mungu pekee ndiye ajuaye.
Hata hivyo ,Magessa anapenda kuwaelezea watanzania kwamba huyo chatu sio wa kweli ni wa kurushwa kwenye fensi yake ili amchafulie  kwani chatu wa ukweli asingeweza kuburuzwa hadi kanisani kwani kila mtu anamwelewa mnyama huyo jinsi alivyo mkali ,kwa hiyo hizo ni njama tu za kuharibiana kwenye maisha .
Hivyo alisema kuwa, kusisitiza kuwa anaombwa watanzania wamwelewe kwani chatu wa ukweli wanafahamika.
ATOA RAI KWA VYOMBO VYA HABARI.
 
Aidha alivitaka vyombo hivyo kuelimisha jamii badala ya kupotosha ukweli wa jambo kama ambavyo sakata hilo limezua sura tofauti kwa watanzania .
‘mnajua nyie ndio vyombo tunavyovitegemea kwa jamii ,sasa mkiandika vitu ambavyo hamna uhakika navyo mnategemea italeta picha gani kwa jamii ya watanzania ‘alisema Magessa.

No comments:

Post a Comment