Sunday, September 7, 2014

DK. KINGWANGALA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS 2015


Na Father Kidevu Blog
Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mbunge wa Nzega Mkoani Tabora, Dk. Hamisi Nassor Kingwangala leo amevunja ukimya na kuweka wazi nia yake ya kuwania nafasi ya Urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani. 

Dk. Kingwangala ametanabaisha hayo hii leo katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam mchana huu katika mkutano wake na vyombo vya habari na Father Kidevu Blog ikiwa miongoni mwao. 

Kufuatia nia hiyo iliyotangazwa na Mbunge huyo Kijana miongoni mwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi si tu kunanesha demokrasia iliyopo ndani ya chama cha mapinduzi bali kunaongeza pia chachu na upinzani miongoni mwa Wabunge vijana walioonesha nia hiyo.

Hadi sasa wabunge kadhaa wa chama cha mapinduzi wameonesha nia hiyo ya kuutaka urasi mwaka 2015 kumrithi Rais Jakaya Kikwete ambapo miongoni mwao ni Mawaziri wa Kuu wastaafu, Frederick Sumaye, Edward Lowassa (MP), pia wapo Bernard Membe, Januari Makamba, Samuel Sitta, Willium Ngeleja huku wengine wakitajwa hivi karibuni, Mizengo Pinda na Mwigulu Mchemba.

No comments:

Post a Comment