WASHINDI TUZO ZA HABARI ZA TANAPA 2013 WAENDELEA KUJIFUNZA MAENEO YA UTALII AFRIKA KUSINI
Mwanahabari
Vedasto Msungu wa ITV (kushoto) na David Rwenyagira (Radio 5) walikuwa
miongoni mwa wanahabari waliofika nje ya Jengo la Mahakama Kuu ya
Pretoria ambapo ilikuwa siku muhimu ya utoaji hukumu kwa mwanariadha
Oscar Pistorius aliyeshitakiwa kwa makosa ya kumuua mpenzi wake kwa
silaha. Unayoyaona hapo nyuma ni magari maalum ya urushaji tukio hilo
moja kwa moja katika vyombo mbalimbali vya habari duniani(OB Van) na
mahema meupe ni Kambi iliyopigwa na wanahabari hao kwa ajili ya
kufuatilia tukio hilo muhimu.
Wanahabari
Vedasto Msungu na David Rwenyagira walipata nafasi ya kumhoji raia huyu
wa Afrika Kusini juu ya maoni yake kwa hukumu iliyotarajiwa kutolewa.
Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 waliweza kufika hadi katika Hifadhi ya
Taifa ya Pilanesberg ili kujionea wanyama mbalimbali. Kutoka Kushoto ni
Mtanzania Peter Masika anayeishi Johannesburg, Vedasto Msungu (ITV),
Pascal Shelutete(Meneja Mawasiliano TANAPA) na Gerald Kitabu wa The
Guardian.
Wanyama aina ya Nyumbu wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Pilanesberg.
Washindi wa Tuzo za TANAPA 2013 waliweza pia kufika katika Mji wa Sun City kama wanavyoonekana hapa.
Washindi wa Tuzo za TANAPA 2013 waliweza kupiga picha na watalii mbalimbali katika jiji la Sun City.
Washindi
wa Tuzo za TANAPA 2013 walikuwa kazini pia kama Vedasto Msungu (kulia)
wa ITV hapa anaonekana akimhoji Mtanzania Peter Masika (kushoto).
No comments:
Post a Comment